Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:18

Bei ya chakula yapanda kote duniani


chakula
chakula

Shirika la chakula duniani FAO, limesema kwamba bei ya chakula imeongezeka kote duniani mwezi Oktoba, kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana kwa mda wa miaka 10 iliyopita.

Shirika hilo limesema kwamba kiwango cha nafaka kote duniani kinatarajiwa kupungua sana.

Bei ya chakula imepanda wa asilimia tatu na kufikia pointi 133.2.

Hii ni mara ya tatu kwa bei ya chakula kupanda na kufikia kiwango cha juu zaidi tangu July 2011.

Bei ya mafuta ya mboga imepanda kwa asilimia 9.6, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kutokea.

Bei ya nafaka ilipanda kwa asilimia 3.2, huku mbei ya unga wa ngano ikipanda kwa asilimia 5, licha ya kuadhimika sokoni kutokana na uzalishaji wa kiwango cha chini.

FAO limesema kwamba licha ya ongezeko la asilimia 0.8 ya uzalishaji wa nafaka mwaka huu, bidhaa hiyo inatarajiwa kuadhimika kote duniani kutokana na ongezeko la mahitaji yanayopanda kwa asilimia 1.7.

Bei ya sukari hata hivyo ilipungua kwa asilimia 1.8 mwezi Oktoba.

Kiwango cha uzalishaji wa nafaka kote duniani kinatarajiwa kufikia tani bilioni 2.793 mwaka 2021.

XS
SM
MD
LG