Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:15

Bunge laepusha uchaguzi mwingine Israel


Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennett
Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennett

Bunge la Israel limepitisha bajeti muhimu ya kitaifa ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa mda mrefu kabla ya siku ya mwisho.

Kukosa kupitishwa kwa bajeti hiyo ingelazimu Israel kuandaa uchaguzi mpya.

Wabunge wamekesha wakijadili bajeti na kuifanyia marekebisho kabla ya kuipitisha alhamisi asubuhi na mapema.

Endapo bajeti hiyo haingepitishwa ifikapo Novemba 14, ingebidhi serikali ya Naftali Benenett, aliyeingia madarakani mwezi Juni kuandaa uchaguzi mkuu ambao ungetoa fursa kwa aliyekuwa Waziri mkuu Benjamain Netanyahu kurejea madarakani.

Israel iliingia katika mgogoro wa kisiasa wa mda mrefu baada ya uchaguzi wa April 2019, wakati chama cha mrengo wa kulia ambacho kilikuwa na ushirikiano na Netanyahu, kukataa kuunda serikali naye wakati alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

XS
SM
MD
LG