Hesabu ya kura inaendelea nchini Afrika kusini katika uchaguzi wa madiwani wa serikali za mitaa.
Uchaguzi huo umetajwa kuwa mtihani kwa umaarufu wa chama kinachotawala cha African national congress ANC.
Chama hicho kilipata asilimia 54 ya kura katika uchaguzi wa manispaa wa mwaka 2016.
Maafisa wa tume ya uchaguzi wanasema hawataraji wapigaji kura wengi kujitokeza kwani hata walojiandikisha walikua wachache.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa baadaye wiki hii.