Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:33

SUDAN: Viongozi waliokuwa wameachiliwa wakamatwa tena


Kiongozi wa jeshi Sudan Jenerali Abdel-Fattah Burhan, Oktoba 26, 2021.
Kiongozi wa jeshi Sudan Jenerali Abdel-Fattah Burhan, Oktoba 26, 2021.

Kiongozi wa chama kilichokuwa kinatawala Sudan Ibrahim Ghandour, amekamatwa kwa mara nyingine tena.

Ghandour alikuwa kiongozi wa chama cha National Congress na Waziri wa mambo ya nje katika serikali ya aliyekuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir.

Familia yake imesema kwamba amekamatwa Jumatatu, saa chache baada ya kuachiliwa huru.

Kuachiliwa kwa Ghandour na viongozi wengine waliokuwa karibu na Bashir, kufuatia mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita, ilikuwa hatua iliyofanyika licha ya pingamizi kubwa kutoka kwa wakosoaji wa utawala wa kijeshi.

Ghandour alikuwa ameshikiliwa kufuatia amri ya jopo kazi lenye mamlaka ya kuharibu msingi uliowekwa na unaoweza kurejesha utawala wa Bashir wa miongo mitatu, ulioanguka mwaka 2019.

Alikuwa ameachiliwa Jumapili usiku, Pamoja na maafisa wawili waliokuwa viongozi wa ujasusi chini ya utawala wa Bashir.

Vyanzo vya habari kutoka idhara ya mahakama vimesema kwamba viongozi wengine wawili waliokuwa karibu sana na Bashir, akiwemo mfanyabiashara Abdelbasit Hamza, walikuwa pia wameachiliwa Jumamosi.

Mwendesha mashataka ya umma naye amefutwa kazi.

Kupitia ujumbe wa facebook, ofisi ya msemaji wa serikali ya Sudan ambayo inahusishwa na serikali ya kiraia iliopinduliwa, ilikuwa imesema kwamba kuachiliwa kwa maafisa hao walitumikia serikali ya Bashir, ilikuwa “hatua inayodhoofisha utendakazi wa taasisi za kulinda mfumo wa sheria.”

XS
SM
MD
LG