Bunge la Uganda limetangaza kwamba wabunge ambao hawajapokea chanjo, hawataruhusiwa kuhudhuria vikao vya bunge hilo kuanzia leo.
Naibu wa spika Anita Among, amesema kwamba hatua hiyo inalenga kutoa mfano mwema katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na janga la virusi vya Corona.
Hatua ya bunge la Uganda inajiri baada ya hatua sawa na hiyo kuchukuliwa na wizara ya afya na mamlaka ya kusambaza dawa nchini humo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema wiki iliyopita kwamba idadi kubwa ya raia wa Uganda wanasita kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona lakini akaeleza matumaini kwamba watu milioni 12 watakuwa wamepata chanjo hiyo kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba kwama huu.
Watu milioni tatu wamepata chanjo hiyo kote Uganda kufukia sasa.
Serikali imeripoti vifo vya watu 3000 kufikia sasa kutokana na virusi vya Corona