Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:11

UGANDA: Shule kufunguliwa Januari 2022


Mwalimu akifunza wanafunzi katika shule ya Everest College wilayani Luwero, Uganda. [Picha: Maktaba]
Mwalimu akifunza wanafunzi katika shule ya Everest College wilayani Luwero, Uganda. [Picha: Maktaba]

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kwamba shule zitafunguliwa mwezi Januari, ikiwa ni karibu miaka miwili tangu shule izlipofungwa nchini humo kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

Museveni amesema kwamba kwamba shule zitafunguliwa bila kujali idadi ya watu watakaokuwa wampokea chanjo wakati huo.

Karibu asilimia 10 ya watu nchini Uganda wamepokea chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona, japo Museveni amesema kwamba kutakuwepo chanjo ya kutosha kwa kila mtu ifikapo mwishoni mwa mwaka hii.

Museveni amesema kwamba raia wa nchi hiyo wataajibika iwapo wanafunzi wataambukizwa virusi vya Corona shule zitakapofunguliwa.

Idadi kubwa ya walimu wameacha kazi ya ualimu na kutafuta kazi zingine ili kujikimu kimaisha na huenda baadhi yao wakakosa kurejea kazini.

XS
SM
MD
LG