Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 19:08

Jeshi la Ethiopia lafanya shambulizi lingine la anga Tigray


Takriban watu sita wameuwawa na wengine 21 wamejeruhiwa katika shambulizi la anga la jeshi la Ethiopia, Alhamisi katika mji mkuu wa Tigray, Mekelle kwa mujibu wa vyanzo vya hospitali vilivyozungumza na VOA.

Shambulizi hilo limefanya jumla ya vifo vilivyo ripotiwa na maafisa wa afya kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ya ndege toka wiki iliyopita kufikia 12 na majeruhi 55.

Jeshi la Ethiopia, lilitoa taarifa ikieleza kwamba shambulizi la sasa lililenga kiwanda cha Mesfin, ambacho kinaelezwa kilikuwa cha matengenezo ya vifaa vya jeshi kilichokuwa kikitumiwa na kundi la TPLF.

Lakini mashuhuda wameiambia VOA kwamba shambulizi hilo la majira ya asubuhi lililenga eneo la makazi ya watu.

Walioshambuliwa walikimbizwa hospitali ya rufaa ya Ayder ambayo ni ya mji, ambapo mmoja wa majeruhi ameiambia VOA kwamba bomu lilishambulia nyumba yake.

XS
SM
MD
LG