Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 16:15

7 wauawa katika maandamano Sudan


Waandamanaji mjini Khartoum, Sudan
Waandamanaji mjini Khartoum, Sudan

Maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan yameingia siku ya nne, waandamanaji wakiweka vizuizi barabarani na wengine kadhaa wakikamatwa.

Waandamanaji saba wamethibitishwa kuuawa tangu jumatatu.

Madaktari na wafanyakazi katika vyumba vya kuhifadhi maiti wamesema kwamba maiti wana majeraha ya kukatwa na vitu vyenye ncha kali.

Maandamano ya mjini Khartoum yameitishwa na muungano wa wataalam nchini Sudan ambao uliandaa maandamano ya mwezi mzima yaliyomuondoa madarakani Omar al-Bashir, April mwaka 2019.

Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha waandamanaji wakipaaza sauti zenye ujumbe wa kutaka utawala wa kiraia.

Waandamanaji hao wamesikika wakiitisha maandamano makubwa jumamosi hii Oktoba 30 na kutaka kiongozi wa mapinduzi Abdel Fattah al-Burhan, kukamatwa na kupelekwa gerezani, alipo Bashir.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni kiongozi mwenye mamlaka makuu Sudan, alivunjilia mbali serikali ya mpito iliyokuwa na majukumu ya kuongoza taifa hilo katika kurejesha utawala wa kiraia.

XS
SM
MD
LG