Brazil inashikilia nafasi ya pili kote duniani kwa idadi ya watu waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Maseneta 7 kati ya 11 wameidhinisha ripoti hiyo baada ya uchunguzi wa miezi sita kuhusu namba serikali ilivyoshughulikia janga la virusi vya Corona.
Kamati hiyo inataka waendesha mashtaka kumfungulia kesi mahakamani rais Bolsonaro kwa makosa kupotosha taifa na uchochezi Pamoja na matumizi mabaya ya pesa za uma.
Anashitakiwa pia kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Kamati imemtaka Bolsonaro kuajibika kwa vifo vya zaidi ya watu 600,000 kutokana na virusi vya Corona.
Rais huyo amekanusha madai yote dhdidi yake.
Uamuzi wa kufungua kesi dhidi ya Bolsonaro umo katika ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu Augusto Aras, aliyeteuliwa na rais Bolsonaro na anayejulikana kwa kumtetea.
Madai ya uhalifu wa kibinadamu yanastahili kuchunguzwa na mahakama ya uhalifu wa kimataifa, ICC.