Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:31

Umoja wa mataifa walaani mapinduzi Sudan, Hamdok aachiliwa huru


Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok akizungumza katika kikao na waandishi wa habari Aug 21 2019 [Picha:maktaba]
Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok akizungumza katika kikao na waandishi wa habari Aug 21 2019 [Picha:maktaba]

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limeshindwa kukubaliana juu ya kulaani mapinduzi ya Sudan yaliyofanyika mapema wiki hii.

Naibu balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Richard Mills amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba mapinduzi hayo hayakubaliki kamwe.

Rais wa baraza hilo Balozi wa Kenya Martin Kimani, akizungumza na waandishi habari amesema wajumbe wengi wamelaani mapinduzi hayo na wametoa wito kwa mataifa kuimarisha juhudi zao kuzuia mapinduzi hayo kuendelea.

Nchini Sudan kwenyewe, Maafisa wa usalama wa Sudan wameanza kuwakamata waandamanaji wanaopinga mapinduzi, na kuamrisha wanajeshi kutumia nguvu.

Jumuiya ya kimataifa imeongeza shinikizo la kutaka kurudi kwa utawala wa kiraia pamoja na kuiadhibu Khartoum . Benki kuu ya Dunia ilisitisha msaada wake kwa Sudan huku Umoja wa Afrika ukisitisha uwanachama wa nchi hiyo kutokana na wanajeshi kuchukua madaraka Jumatatu.

Mwenyekiti wa baraza huru la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, akizungumza na waandishi wa habri mjini Khartoum jumanne, alisisitiza kwamba japo viongozi wa kijeshi na wa kiraia walikuwa wamefanya mazungumzo tangu kuundwa kwa serikali ya mpito mwaka 2019, kulikuwepo tofauti kati ya waakilishi hao, huku baadhi ya waakilishi wakiwemo baadhi ya wanajeshi wakitengwa katika mazungumzo hayo.

Amesema kwamba hatua ambayo imechukuliwa na wanajeshi, inalenga kutengeneza mambo ambayo yamaeharibika na wala sio kuanzisha mapinduzi ya kijeshi.

"Tunataka kuunda serikali ya kiraia ambayo iatatekeleza jukumu kubwa wakati wa kipindi hiki cha mpito. Japo baadhi ya sehemu za katiba zimepigwa marufuku kwa sasa, tutazingatia sana katiba. Tunataka kuunda serikali itakayowaridhisha raia wote wa Sudan.” Amesema al-Burhan.

Ofisi ya serikali yampito ya Sudan nayo imetoa taarifa inayosisitiza kwamba serikali ya Hamdok inatambuliwa na watu wa Sudan na dunia kwa jumla.

Hamdock ameachiliwa huru na kurudi nyumbani kwake jumanne jioni lakini baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaendelea kuzuiliwa na jeshi.

Maelfu ya waandamanaji wanaendelea kujitokeza barabarani tangu jumatatu kupinga mapinduzi hayo ya kijeshi yaliyoongozwa na kamanda wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan.

Watu kadhaa wameuawa katika makabiliano na maafisa wa usalama.

Miungano na wanaharakati wameitisha maandamano makubwa mjini Khartoum, jumamosi.

XS
SM
MD
LG