China imeripoti kwa shirika la afya duniani, kwamba wananchi wake 21 wameambukizwa na homa ya ndege mwaka huu, ikilinganishwa na watu 5 mwaka uliopita.
Japo idadi ya maambukizi ni ya chini ikilinganishwa na mamia ya watu walioambukizwa homa ya ndege mwaka 2017, maambukizi hayo yanaripotiwa kuwa mabaya sana na yanafanya watu kuwa wagonjwa sana. watu sita wamefariki duniani kutokana na homa ya ndege nchini China.
Visa vingi vilivyoripotiwa ni watu waliokaribia ndege wa kufungwa nyumbani, lakini hakuna kesi imethibitishwa ya maambukizi kutoka kwa biandamu hadi kwa binadamu.
Shirika la afya duniani WHO, limesema kwamba uchunguzi zaidi unahitajika kufanyika kwa haraka ili kuelewa maambukizi hayo na kuyadhibithi.