Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:35

Mpwa wa mfalme aamua kuishi maisha ya mtu wa kawaida


Mako na mme wake Kei Komuro
Mako na mme wake Kei Komuro

Mpwa wa mfalme wa Japan, Mako, ameolewa na mchumba wake wa tangu chuo kikuu na kuachana na hadhi yake ya ufalme, akisema kwamba anataka kujenga maisha yenye furaha na mme wake.

Katika kikao na waandishi wa habari na mme wake Kei Komero ambaye ni ria wa kawaida, Mako amesema kwamba ndoa yake haingezuiliwa licha ya pingamizi kadhaa.

Mako, ambaye sasa anatambuliwa kama Mako Komuro, aligunduliwa kuwa na msongo wa mawazo mapema mwaka huu baada ya kuposwa na kusababisha Sakata la kifedha Pamoja na kuangaziwa sana na vyombo vya habari Pamoja na kutenganishwa na mchumba wake kwa miaka mitatu.

Kwa kawaida, ndoa za kifalme hufuata kanuni za kifalme lakini wawili hao hawakufuata kanuni hizo na hata walikataa dola milioni 1.3 zinazotolewa kwa wanwake wanaoondoka katika familia.

Wawili hao wataishi New York, Marekani na Mako ameomba passipoti ya usafiri kwa mara ya kwanza.

XS
SM
MD
LG