Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:55

Mali yamfukuzwa mjumbe wa ECOWAS


Mwanajeshi wa Mali karibu na mto Niger, Mopti [picha ya maktaba]
Mwanajeshi wa Mali karibu na mto Niger, Mopti [picha ya maktaba]

Serikali ya mpito ya Mali imemfukuza mwakilishi wa jumuiya ya uchumi wa nchi za Afrika magharibi Ecowas. Tarifa ya serikali inaeleza kwamba Hamidou Boly amepewa saa 72 kuondoka nchi hiyo kwa sababu za hatua zake zisizoambatana na wadhifa wake.

Kulingana na taarifa ya serikali iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, serikali ya Mali imeamua kutangaza kwamba mwakilishi maalum wa jumuiya ya uchumi wa nchi za Afrika magharibi ECOWAS, hakubaliwi nchini humo.

Taarifa hiyo inasema kuwa umauzi huo umechukuliwa kutokana na hatua anazochukua zinazokinzana na hadhi yake.

Hakuna taarifa kamili kueleza zaidi kuhusu kilichopelekea hatua hiyo kuchukuliwa.

Hata hivyo, hatua hiyo inajiri wakati viongozi wa kijeshi wa Mali wanakabiliwa na shinikizo kubwa la kutaka kukabidhi madaraka kwa raia.

Mabalozi wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikutana mwishoni mwa wiki na viongozi wa kijeshi na kusisitiza juu ya haja ya kurudishwa kwa utawala wa kiraia kwa haraka iwezekanavyo.

Mali iliingia katika mgogoro wa kisiasa Agosti mwaka uliopita, kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Kanali Assimi Goita dhidi ya rais Ibrahim Boubacar Keita.

Uongozi wa kisiasa uliunda serikali ya mpito kufuatia shinikizo la kimataifa kuwekewa vikwazo.

Serikali ya mpito ilipewa majukumu ya kuhakikisha kwamba utawala unarejea mikononi mwa raia chini ya mfumo wa demokrasia.

Lakini Goita aliwafukuza viongozi wote wa serikali hiyo ya mpito mnamo mwezi May na kujitangaza kuwa rais wa mpito, hatua iliyokoselewa sana kimataifa.

Serikali ya mpito ya Mali imesema kwamba itatangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu baada ya kuandaa kongamano la kitaifa mwezi Desemba, kuhusu namna ya kujenga upya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG