Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 14:42

Wanawake wajawazito wadaiwa kunyanyaswa hospitalini Msumbiji


Makundi ya haki za binadamu ya Msumbiji yameshutumu hospitali za serekali kwa manyanyaso na kulazimisha wajawazito kulipia huduma za uzazi ambazo zinapaswa kuwa bure.

Kundi la asasi za kiraia 40 zilizo jiunga chini ya mwamvuli wa Umoja wa Uangalizi wa Wanawake wiki hii, limesema kwamba limepokea ripoti16 za manyanyaso, na usumbufu kutoka hospitali za umma ambazo zinapaswa kuwa bure ndani na nje ya mji mkuu wa Maputo toka kuanza kwa mwaka 2021.

Wote ambao wameshindwa kulipia huduma hizo hawakupata huduma, na wamenyanyaswa kwa mujibu wa madai ya makundi hayo.

Katika taarifa iliyo tolewa Jumatatu na kundi hilo la uangalizi, waathirika wamesema walitakiwa kulipia dola 50 ili kupata matibabu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG