Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:25

Jeshi na Polisi wapelekwa shuleni kuzuia maandamano Eswatini


Picha ya maktaba ikionyesha ghasia za maandamano Eswatini.
Picha ya maktaba ikionyesha ghasia za maandamano Eswatini.

Makundi yanayo tetea demokrasia katika taifa la kusini mwa Afrika, Eswatini, yanaeleza kwamba serekali imepeleka wanajeshi na polisi katika shule ambazo wanafunzi wamekuwa wakiendelea na maandamano kwa wiki kadhaa wakitaka mageuzi ya kisiasa.

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika taifa ambalo zamani lilifahamika kwama Swaziland, na taifa pekee la Kiafrika lenye utawala kamili wa kifalme, wamesusia masomo na wamekuwa wakiandamana kwa amani.

Madai yao ya msingi ni kuachiliwa waandamanaji wawili wanao tetea demokrasia, ambao walikamatwa mwanzano mwa mwaka huu, pia wanahitaji mazingira bora ya kusomea, na elimu iwe bure.

Msemaji wa kundi moja la kutetea demokrasia la Swaziland Solidarity Network, Lucky Lukhele, amesema wanajeshi walipelekwa katika shule hizo ili kuwatisha wanafunzi lakini hawakudhuru wanafunzi hao.

Licha ya hayo, amedai wanafunzi 17 ikijumuisha wale wenye umri wa miaka 7 walikamatwa katika maandamano ya Jumatatu.

Msemaji wa jeshi Tengetile Khumalo, amethibitisha jeshi kupelekwa katika shule ambazo wanafunzi wanaandamana.

XS
SM
MD
LG