Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 04:43

Papa Francis akutana na mtawa aliyetekwa Mali


Papa Francis Jumapili alikutana na Gloria Cecilia Narvaez, mtawa wa Kifrancisca kutoka Colombia.

Tukio hilo limefanyika siku moja baada ya mtawa huyo kuachiliwa na wanamgambo wenye msimamo mkali wa Mali.

Alishikiliwa kwa zaidi ya miaka minne kwa mujibu wa msemaji wa Vatican.

Mtawa Gloria alitekwa Febuari 7, 2017 kusini mwa Mali karibu na mpaka wa Burkina Faso ambako alikiwa akilitumikia kanisa.

Ofisi ya rais wa Mali ilitangaza kwamba mtawa Gloria aliachiliwa Jumamosi, na kumpa pole kwa ujasiri wake aliokuwa nao kwa kipindi chote hicho.

Kabla ya Papa ya kufanya ibada ya umma Jumapili, alimsalimu mtawa huyo wa Colombia kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vatican.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG