Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:28

Mkenya Peres Jepchirchir ashinda dhahabu ya Marathon kwenye Olimpiki


Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mbio za Marathon kwenye Olimpiki nchini Japan.
Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mbio za Marathon kwenye Olimpiki nchini Japan.

Peres Jepchirchir wa Kenya alipambana na joto kali na unyevu siku ya Jumamosi nchini Japan, na kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki, katika mbio za Marathon za wanawake kwa kumaliza kwa muda wa saa mbili, dakika 27 na sekunde 20.

Aliyechukua nafasi ya pili, na hivyo kupata medali ya fedha ni Mkenya mwenzake, Brigid Kosgei, kwa kumaliza mbio hizo kwa saa 2, dakika 27 na sekunde 36.

Mmarekani Molly Seidel, alishika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2, dakika 27 na sekunde 46.

Waandaaji wa Olimpiki walianzisha mbio za marathon za wanawake saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Japan, saa moja mapema kuliko ilivyopangwa, katika juhudi za kuwakinga wanariadha na joto kali na unyevu.

Chechirchir asherehekea ushindi baada ya kukabidhiwa medali ya dhahabu.
Chechirchir asherehekea ushindi baada ya kukabidhiwa medali ya dhahabu.

Wanariadha kumi na tano kati ya 88 hawakumaliza mbio hizo, zilizofanyika katika mji wa pwani wa Sopporo, karibu kilomita 1,100, kaskazini mwa Tokyo.

Kosgei, anayeshikilia rekodi ya dunia, na bingwa mwingine Ruth Chepngetich, ambaye pia ni raia wa Kenya, walitarajiwa kushinda dhahabu leo Jumamosi, lakini Chepngetich alishindwa kumaliza mbiyo hizo. Jepchirchir alimpita Kosgei karibu na mwisho wa mbio hizo, katika kilomita ya arobaini.

XS
SM
MD
LG