Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:27

Wananchi wa Zanzibar wafurahia kuachiwa viongozi wa Uamsho


Sheikh Farid Hadi Ahmed kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar
Sheikh Farid Hadi Ahmed kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar

Hali ya furaha imetanda visiwani Zanzibar siku ya Jumatano baada ya kuachiwa huru na kufika Zanziba masheikh saba wa Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu Zanzibar, JUMIKI. hata hivyo mmoja wa wakili wao anasema hakuarifiwa juu ya sababu au kushirikishwa katika kuachiwa kwa viongozi hao.

Masheikh Farid Hadi Ahmed na Msellem Ali Msellem walirudishwa Zanzibar Jumanne, magharibi baada ya kuachiwa huru mjini Dar Es Salaam, kufuatia uwamuzi wa mkurugenzi wa mashtaka wa Tanzania Sylvester Mwakitalu kuwafutia mashtaka dhidi yao.

Wanachama wengine watano wamewasili Zanzibar Jumatano mchana ikiaminika kwamba wanaachiwa kwa makundi kama alivyosema kiongozi wao Sheikh Farid Ahmed aliyeachiwa Jumanne.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, moja wapo ya wakili wa Masheikh hao, Abdallah Juma anasema wamefurahi kuwaona nyumbani lakini wanadhani wao mawakili wangelishirikishwa kwenye utaratibu wote wa kuachiwa huru wateja wao baada ya kuwawakilisha kwa zaidi ya miaka 9.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:45 0:00

Masheikh hao pamoja na wafuasi wao wapatao 50 walikua wanashikiliwa gerezani kwa makosa ya ugaidi na walifunguliwa mashtaka mwaka 2014. Miongoni mwa mashtaka hayo ni pamoja na kuwaingiza watu kutoka nje kushiriki kwenye vitendo vya ugaidi. Tuhuma ambazo wote wanakanusha.

Wachambuzi wa mambo Zanzibar wanasema kuachiwa kwa viongozi hao wa kislamu huwenda inafuatia mazungumzo aliyokua nayo rais Hussein Mwinyi na viongozi wa kidini juuu ya hatima ya wanachama wa Jumiki.

XS
SM
MD
LG