Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 16:52

Meli iliyoziba mfereji wa Suez yashikiliwa baharini


Meli ambayo ilikiwa imeziba mfereji wa Suez kwa takriban wiki moja mwezi Machi inashikiliwa baharini wakati huu.

Mamlaka za mfereji wa Suez inataka kulipwa fidia ya dola milioni 916 kutoka kwa kampuni ya Japan inayo miliki meli hiyo.

Taarifa hizo zimetolewa na moja ya makampuni ya bima ya meli hiyo na vyanzo vingine vya kutoka katika mamlaka za mfereji wa Suez na kuripotiwa na shirika la habari la Reuters Jumanne.

Meli ya Ever Given inayo milikiwa na Shoei Kisen imekuwa katika maeneo mawili ya maji yanayo gawanyisha mfereji wa Suez toka ilipo tolewa Machi 29, huku mamlaka ya mfereji wa Suez (SGA) ikifanya uchunguzi.

Vyanzo viwili vya SGA vilivyo kataa kutambulishwa vimeiambia Reuters kwamba amri ya mahakama imetolewa kuishikilia meli hiyo.

Mazungumzo juu ya fidia yanaendelea kwa mujibu wa moja ya vyanzo vya taarifa hii.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG