Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 16:36

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake kutosafiri Kenya


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Washington DC

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imewaonya wamarekani kutosafiri nchini Kenya kwa wakati huu, kutokana na janga la Covid-19, uhalifu, ugaidi na utekaji nyara.

Taarifa ya tahadhari ambayo imetolewa na wizara hiyo inawashauri wamarekani kutojielekeza kwenye eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia na kwenye maeneo ya pwani kutokana na ugaidi.

Wizara hiyo imewasihi raia wa Marekani kuchukua tahadhari kubwa wanaposafiri nyakati za usiku kila mahali nchini humo kwa sababu za uhalifu, pia wajiepushe kwenda mitaa ya Eastleigh na Kibera, mjini Nairobi kutokana na vitendo vya uhalifu na utekaji nyara.

Uhalifu mbaya kama vile wizi wa magari kwa kutumia silaha, uvamizi wa majumbani na utekaji nyara, unaweza kutokea wakati wowote, taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje imesema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG