Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:12

Nana Akufo-Addo aapishwa kwa mhula wa 2 Ghana, wabunge wapigana


Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo

Rais wa Ghana Akufo-Addo, ameapishwa kama rais kwa mhula wa pili madarakani, siku moja baada ya kutokea vurugu bungeni.

Akufi – Addo alimshinda mpinzania wake rais wa zamani John Mahama katika uchaguzi uliofanyika mwezi Desemba na ambao ulikuwa na ushindani mkali sana.

Wabunge wa Ghana, ambao walichaguliwa hivi karibuni walipigana bungeni baada ya kukosa kukubaliana namna ya kumteua spika.

Uchaguzi wa spika ulikuwa umepangwa kufanyika kwa njia ya siri, lakini wabunge kutoka chama kinachotawala cha New Patriotic NPP, walikuwa wakionyesha hadharani waliyempigia kura, jambo ambalo liliwakera wabunge wa upinzani.

Wakati mmoja, mbunge wa chama kinachotawala alichukua karatasi za kupigia kura kwa lazima wakati uchaguzi ulikuwa unaendelea na hivyo kuzua mgogoro.

Polisi wenye silaha na wanajeshi wameitwa bungeni katika juhudi za kurejesha utulivu.

Chama kinachotawala na upande wa upinzani, wana idadi sawa ya wabunge. Kuna mbunge mmoja asiyekuwa na chama cha kisiasa.

Mahakama ilimzuia mmoja wa wabunge wa upinzani kushiriki katika kura hio ya kujaza nafasi ya spika, baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani kupinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu. Mbunge huyo hata hivyo alikubaliwa na bunge kushiriki uchaguzi huo.

Wanasiasa wa upinzani wamedai kuwepo udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi Desemba na wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu kabisa kutaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG