Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 07:03

Waasi wamedhibithi sehemu kadhaa za Jamhuri ya Afrika ya kati huku matokeo ya uchaguzi yakiendelea kutolewa


Wanajeshi wa umoja wa Afrika wanaolinda amani Jamhuri ya Afrika ya kati

Makundi ya waasi yanaendelea kudhibiti sehemu za kusini mwa mji wa Bangassou, Jamhuri ya Afrika ya kati, wiki kadhaa baada ya kushutumiwa kwa kujaribu kupindua serikali, huku matokeo ya uchaguzi mkuu yakiendelea kutolewa.

Kundi la wapiganaji ambalo linadhibithi theluthi tatu ya Jamhuri ya Afrika ya kati, lilianza mashambulizi dhidi ya serikali mnamo Desemba 19 kwa lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu na kutwaa mji mkuu wa Bangui.

Wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa na wa Rwanda, wamewazuia kuingia mji mkuu.

Hata hivyo, wapiganaji hao wameshambulia mji wa Bangassou, wenye madini ya almasi, karibu na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kilomita 750 kutoka mji mkuu wa Bangui.

Wapiganaji watano waliuawa na wanajeshi wawili kujeruhiwa katika shambulizi hilo la jumamosi.

Taarifa ya muungano wa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa nchini humo - MINUSCA, umesema kwamba wapiganaji hao wanamuunga mkono aliyekuwa rais Francois Bozize.

Serikali ya rais Faustin Archange Touadera – anayetarajiwa kushinda uchaguzi uliofanyika Desemba 27, imemshutumu Bozize kwa kujaribu kufanya mapinduzi.

Bozize amekanusha madai hayo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG