Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:36

Kura zahesabiwa Jamhuri ya Afrika ya kati, kuna wasiwasi mkubwa wa kutokea mashambulizi


Waangalizi wa uchaguzi kutoka umoja wa Afrika, jumuiya ya uchumi wa mataifa ya Afrika ya kati, na wa kutoka ukanda wa Sahel, wamesema uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati uliofanyika jumapili iliyopita, kuwa hatua muhimu sana iliyoimarisha demokrasia ya nchi hiyo.

Waangalizi hao walifuatilia uchaguzi huo katika miji miwili pekee kutokana na wasiwasi wa ukosefu wa usalama kutokana na tisho la makundi ya waasi kufanya mashambulizi.

Uchaguzi huo wa Jumapili ni hatua muhimu sana kwa nchi hiyo yenye misukosuko mikubwa ya usalama, kiwango kikubwa cha umaskini na mashambulizi ya kila mara kutoka kwa makundi ya waasi.

Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na vita vya kila mara tangu kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Makundi ya waasi yanashikilia theluthi tatu ya nchi hiyo na kura zimesafirishwa hadi mjini Bangii ili kuhesabiwa.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yatatolewa Januari 18.

Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Februari 14 iwapo mshindi hatakuwa amepatikana katika duru ya kwanza.

Kamati ya serikali kuhakilisha kwamba uchaguzi huo unakuwa huru na haki, imesema kwamba uchaguzi haukufanyika katika wilaya 12.

XS
SM
MD
LG