Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:01

Chanjo ya AstraZeneca yaidhinishwa Uingereza


Chanjo dhidi ya kirusi cha corona iliyotengenezwa na kampuni ya AstraZeneca, kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Oxford, imeidhinishwa kwa matumizi nchini Uingereza.

Dozi ya kwanza ya chanjo hiyo itatolewa jumatatu, wakati maambukizi ya virusi vya Corona yameendelea kuongezeka kwa kasi nchini Uingrereza.

Uingereza imeagiza dozi milioni 100 za chanjo hiyo, ambazo zinatosha watu milioni 50.

Waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock amesema kwamba kiasi cha chanjo ambayo imeagizwa na Uingereza, kinatosha watu wote nchini Uingereza. Kiasi hicho ni Pamoja na dozi zilizoagizwa kutoka kwa kampuni ya Pfizer BioNTech.

Uingereza inatarajiwa kurejesha masharti makali ya kusitisha shughuli za kawaida katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ili kudhibithi maambukizi.

Zaidi ya watu 53,000 waligunduliwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Uingereza jana Jumanne.

Watu 414 wamefariki dunia katika siku 28 zilizopita.

Waziri mkuu wa Uingereza Borris Johnson ametaja hatua ya kupatikana kwa chanjo ya AstraZeneca kuwa ufanisi mkubwa kwa wanasayansi wa Uingereza.

XS
SM
MD
LG