Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 07:33

Miaka 10 ya mapinduzi ya nchi za kiarabu Arab Spring hayajaleta mageuzi yaliyotarajiwa


Miaka 10 iliyopita Disemba 17, 2010 Mohamed Bouazizi mchuzi wa matunda nchini Tunisia alijitia moto na kifo chake kikasababisha mapinduzi makubwa kuwahi kushuhudiwa katika nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Kilichopatikana miaka 10 baada ya mapinduzi ya nchi za Kiarabu
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:50 0:00

Mapinduzi hayo yaliyofahamika kama 'Arab Spring' yaliwaondowa madarakani viongozi wa kimabavu wa nchi za kiarabu kuanzia Zine El-Abidine Ben Ali wa Tunisia, Husni Mubarak wa Misri, Muammar Ghadafi wa Libya hadi Ali Saleh wa Yemen.

Wachambuzi, wanaharakati na waandishi habari katika kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wanasema matumaini makubwa yaliyokuwepo kutokana na mapinduzi yaliyongozwa na vijana kuanzia Tunisia, kupitia Misri kuelekea Libya, Yemen na hatimae Syria, ya kupigania mageuzi ya kijamii, uhuru wa kisiasa na kujieleza yalitoweka muda mfupi tu baada ya kuanza.

Mapinduzi katika nchi hizo yalifanikiwa kuwaondosha viongozi wa muda mrefu wa nchi hizo lakini ni Tunisia pekee ambako kuna ishara za mafanikio kidogo pale utawala wa kidemokrasia umeanza kuota mizizi.

Arshid Adib-Moghaddam Profesa katika chuo cha London cha taaluma ya Afrika na mashariki ya kati SOAS, akizungumza na shirika la habari la AFP anasema wananchi wa kanda ya Mashariki ya kati wameweka kipmo cha kisiasa ambapo katika baadhi za nchi hawakufanikiwa na baadhi kuna matumiani makubwa bado kama Tunisia.

"Nchini Tunisia, mapinduzi ya Arab Spring yalileta mafanikio kwa vile yameweza kubuni taasisi za utawala na taifa ambalo linafuata misingi ya kidemokrasia na kuwajibika kwa raia wake," amesema Adib-Moghaddam

Katika kipindi cha miaka kumi watunisia wameidhinisha katiba mpya na kumekuwepo na uchaguzi wa rais mara mbili na kumchagua mwanasiasa asiyejulikana Kais Saied mwaka jana kwa kutoridhika na vyama vya kisiasa pamoja na mara mbili kuchagua wabunge ambao wamegawiga zaidi kuliko ilivyokua miaka 10 iliyopita na na si watu wengi wenye kusherehekea siku hii ya leo.

Hata hivyo hali ya uchumi na kijamii haijabadilika kamwe, na janga la Covid-19 waatalamu wanasema limezidisha maisha kua magumu.

Lakini maisha yao ni bora kuilko ilivyo katika mataifa jirani yaliyoshuhudia mapinduzi kuanzia Libya, Misri Yemen hadi Syria. Nchini Libya baada ya miaka 10 ya mapigano angu kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Ghadafi kutokana na msaada wa ushirika wa Nato, wajumbe wa pande mbili wamefikia makubaliano ya kuunda serikali. Wajumbe wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa mjini Tripoli imefikia makubaliana na wale wa serikali ya Mashariki inayoungwa mkono na jenerali aliyeas Khalifa Haftar.

Ahmed Kadhaf al-Dam BInamu na aliyekua mshauri wa karibu wa Muamar Ghadafi anaishi cairo, ameliambia shirika la habari la Afp kwamba haamini kulikuwepo na mapinduzi ya kweli ya wananchi.

"Yale ambayo yamekua yakitokea mnamo miaka 10 iliyopita, uharibifuwa mali, mauwaji, watu kukoseshwa makazi, na ugaidi pamoja na uhamiaji haramu ni jibu la wazi kwamba hapakuwepo na mapinduzi ya Arab Spring . kilichokuwepo ni shambulizi la Nato la kumua Muammar Ghadafi," amesema Kadhaf al-Dam

Nchini Yemen ambako kiongozi wa muda mrefu Ali Saleh ambae pia aliondolewa kwa malalamiko ya wananchi mapigano yangali yanndelea na taifa hilo linatajwa kua na janga kubwa la binadamu kuwahi kutokea na shirika la hisani la International Rescue Committee IRC.

Ingawa vijana wa Misri walifanikiwa kumondoa kiongozi wa muda mrefu Housni Mubarak, lakini jeshi halijakubali mabadliko ya kidemokrasia.

Mohamed Lotfy mkurugenzi mtendaji wa kamisheni ya haki na uhuru ya misri ECRF anasema srikali ya misri inafanya kila iwezako kutokoweza ndoto ya mapinduzi ya Januari 25

"Miaka kumi baadae tumerudi nyuma, ingawa tungali tunaona matumaini miongoni mwa vijana. Lakini serikali inafanya kila njia kukandamiza watu kwa kukiuka haki za binadamna kutoshtahmilia ukosoaji wa mtu yeyote," amesema Lotfy.

Ingawa ndoto ya kubadili ukurasa katika nchi za kiarabu iliyojitokeza miaka kumi iliyopita imetoweka kwa sehemu fulani, lakini matumaini yanaonekana yagali yapo, kufuatia mapinduzi ya Algeria na Sudan yaliyofanyika karibu miaka minnae baada ya mapinduzi ya awali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG