Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:33

Maambukizi ya Corona yaongezeka kwa kasi Ulaya


Mipaka ya nchi za Ulaya bado iko wazi kwa sasa
Mipaka ya nchi za Ulaya bado iko wazi kwa sasa

Nchini Uingereza watu 16,982 wamedhibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona ndani ya siku moja. Serikali za mitaa zimeanza kutekeleza masharti makali ya kudhibiti maambukizi.

Serikali ya Wales imetangaza kusitishwa kwa shughuli za kawaida kufuatia kuongezeka kwa kasi kwa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona.

Shughuli za kawaida zitasitishwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia Ijumaa, kila mtu akihitajika kusalia nyumbani isipokuwa wafanyakazi muhimu kabisa kama wahudumu wa afya.

Waziri Mkuu Mark Draneford amesema kwamba anaelewa kuwa watu wamechoshwa na masharti ya kukabiliana na maambukizi lakini masharti hayo ni muhimu sana kwa wakati huu, katika kupambana na virusi vya Corona.

“Inatulazimu kuchukua hatua za haraka na dhabitho ili kupata matokeo tunayohitaji. Kila mtu nchini Wales anatakiwa kusalia nyumbani. Iwapo hatutafanya hivyo sasa, maambukizi yataendelea kuongezeka” amesema Dreaneford.

Kila mtu, isipokuwa wafanyakazi mkuhimu kabisa watafanyia kazi nyumbani.

Biashara zote zitafungwa kuanzia Ijumaa hadi Novemba 9.

Maambukizi yaongezeka Uingereza, Scotland

Nchini Uingereza watu 16,982 wamedhibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona ndani ya siku moja. Serikali za mitaa zimeanza kutekeleza masharti makali ya kudhibiti maambukizi.

Maafisa wa serikali wameshindwa kukubaliana namna ya kukabiliana na wimbi jipa la maambukizi, Waziri Mkuu Borris Johnson akishutumiwa namna anavyoshughulikia wimbi hilo jipya la virusi vya Corona.

Scotland imeanza kutekeleza mikakati kadhaa ya kupambana na virusi hivyo, raia wake wakitakiwa kufuata maagizo ya maafisa wa afya kwa lazima.

Amri ya watu kufanya kazi wakiwa nyumbani kwa muda wiki nne itaanza kutumika kuanzia Ijumaa wiki hii.

Sehemu ya Ujerumani yafungwa kwa kwa mara ya pili

Katika wilaya ya Bavaria nchini Ujerumani, shughuli za kawaida zimefungwa kwa mara ya kwanza tangu mwezi April, kila mtu akitakiwa kusalia nyumbani kwake.

Watakaondoka nyumbani kwao wanatakiwa kuwa na sababu ya msingi.

Shughuli katika wilaya hiyo zitafungwa kwa muda wiki mbili kuanzia Jumanne, saa nane kamili mchana sasa za Ujerumani.

Bavaria inakuwa sehemu ya kwanza kurejea katika hatua ya kufunga shughuli za kaiwaida kwa mara ya pili nchini Ujerumani tangu mwezi April.

Jumla ya watu 7830 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona kila siku, nchini Ujerumani.

Kansela wa ujerumani Angela Markel amehimiza watu kutosongeana na kupunguza safari zisizo na umuhimu mkubwa.

Masharti makali zaidi yatangazwa Ireland

Ireland imetangaza mojawapo ya masharti makali zaidi ya kupamba na maambukizi ya virusi vya Corona barani Ulaya.

Migahawa, baa na biashara zimefungwa kuanzia Jumatatu huku safari za umbali wa kilomita 5 kutoka nyumbani kwao zikipigwa marufuku.

Hata hivyo, shule zitaendelea kufunguliwa na shughuli za ujenzi kuendelea.

Waziri Mkuu Micheal Martin amesema kwamba masharti hayo ataendelea kutumika kwa mda wa wiki sita.

Karibu watu milioni 1 waambukizwa Spain

Idadi ya maambukizi ya Corona nchini Spain imeongezeka kwa kasi na kufikia watu 974,449 kufikia Jumatatu.

Wizara ya afya imesema kwamba wafu 33,992 wamefariki kufikia sasa.

Nchi hiyo imekuwa ikiripoti visa 12,000 vya maambukizi ya Corona kia siku katika wiki za hivi karibuni.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG