Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:35

Trump aamrisha jeshi kushambulia chombo cha Iran kinachosababisha kitisho kwa manowari zake


Boti za Jeshi la Kulinda Maoinduzi ya Iran zikipita karibu na manwari ya messi la Maremmani fatica Ghuba ya uwajemi April 15, 2020
Boti za Jeshi la Kulinda Maoinduzi ya Iran zikipita karibu na manwari ya messi la Maremmani fatica Ghuba ya uwajemi April 15, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump, ameagiza jeshi la Marekani kushambulia na kuharibu kabisa meli za kivita za Iran, endapo zitaendelea kufanya kile ametaja kuwa uchokozi dhidi ya meli zake katika Ghuba ya Uwajemi.

Agizo hilo limetokea wiki moja baada ya meli 11 za kikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi wa Iran kusongea karibu sana na meli za Marekani katika Ghuba ya Uwajemi.

“Nimeaagiza jeshi la Marekani kushambulia na kuharibu meli yoyote na za Iran, endapo zitachokoza meli zetu baharini” ameandika Trump kwenye twiter, saa chache baada ya kikosi cha ulinzi cha jeshi la Iran kusema kwamba kimeafirisha satellite ya kijeshi katika anga za juu.

Roketi inayosafirisha seteliti ya Iran, Nour, kuelekea anga za juu
Roketi inayosafirisha seteliti ya Iran, Nour, kuelekea anga za juu

Mzozo kati ya meli za kivita za Iran na za Marekani, ulikuwa jambo la kawaida kati ya mwaka 2016 na 2017, wakati jeshi la Marekani lilifyetua risasi kadhaa hewani kutahadharisha meli za Irani dhidi ya kuzisongea.

Japo jeshi la Marekani lina mamlaka ya kuchukua hatua za kujilinda, matamshi ya Trump yanaonekana kuashiria uwezekano wa kutokea mgogoro zaidi kati ya Iran na Marekani.

Afisa wa ngazi ya juu wa Pentagon, amesema matamshi ya Trump kuhusu Iran yamechukuliwa kama onyo kwa Tehran, lakini akapendekeza kwamba jeshi la Marekani litaendelea kufanya kazi yake kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuchukua hatua za kujilinda.

“Rais alitoa onyo muhimu kwa Iran. Kile alikuwa anasisitiza ni kwamba meli zetu zina haki ya kujilinda dhidi ya uchokozi”, amesema kaimu waziri wa ulinzi David Norquist, katika kikao na waandishi wa habari, Pentagon siku ya Jumatano.

Msemaji wa jeshi la Iran Abolfzl Shekarchi, amesema kwamba Trump anastahili kuangalia namna ya kuokoa wanajeshi wake na janga la Corona.

Matamshi yake yametolewa mda mfupi baada ya agizo la Trump.

Mgogoro kati ya Iran na Marekani uliongezeka mapema mwaka huu baada ya Marekani kumuua mkuu wa usalama wa Iran, Qassem Soleimani, katika shambulizi la Roketi nchini Iraq.

Imetaarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG