Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 19:39

Sultan mpya wa Oman aahidi kuendelea na sera za aliyemtangulia Sultan Qaboos


Sultan Haitham wa Oman aahidi kuendelea na sera za Sultan Qaboos
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:26 0:00

Kiongozi mpya wa Oman Haitham bin Tariq al Said, ameahidi kuendelea na sera za kigeni za taifa hilo la kifalme ambazo anasema zilijengwa na Sultan Qaboos, chini ya misingi ya kuishi kwa amani na majirani zake na kuendeleza ushirikaino wa kirafiki na mataifa ya dunia

"Sultan Qaboos bin Said bin Taimur, Mwenyezi mungu amlaze pema, alikua mtu ambae hotuba kama hii ninayo itoa haiwezi kufafanua kwa dhati kile alichofanikiwa kufanya na kujenga. Amejenga taifa la kisasa linalotambuliwa na wakosowaji kabla ya wapenzi wake. Na amebuni kipindi cha kihistoria ambacho kinaweza kushuhudiwa kutokana na mfumo wa sheria na utawala ambao unaloliongoza taifa na kufungua njia kwa mustakbali wa mafanikio aliyo kua na ndoto kuona imestawi". alisema Sultan al Said

Katika hotuba hiyo yake, Haitham alitoa wito pia kuendelea na juhudi za kujenga zaidi taifa hilo dogo lenye utajiri wa mafuta na kuendelea na njia iliyopangwa na aliyemtangulia Sultan Qaboos aliyefariki Ijuma.

Haitham anachukua madaraka akikabiliwa na changamoto kubwa za ndani ya nchi kutokana na hali ngumu ya kifedha, ukosefu mkubwa wa ajira, madeni na hasa wakati wa mvutano mkubwa kati ya Iran na Marekani. Kabla ya sherehe hizo maafisa wa serikali kupitia televisheni ya taifa wamesema walifanya uteuzi huo baada ya kufungua barua ya Saultan Qaboos iliyomtaja binamu wake kuchukua nafasi yake bila ya kutoa maelezo zaidi.

Tangazo hilo lilitolewa wakati Wa-Omani walisimama katika njia za mji mkuu wa Muscat kutoa heshima zao za mwisho pale jeneza la Qaboos al Said ilipokua inapita.

Sultan wa amani wa Oman Qaboos bin Said al-Said
Sultan wa amani wa Oman Qaboos bin Said al-Said

Qaboos alitawala taifa la kale la kifalme la Mashariki ya kati akichukua madaraka 1970 kutokana na mapinduzi ndani ya kasri ya mfalme. Alifahamika kimataifa kwa msimamo wake wa kidiplomasia wa kutopendelea upande wowote katika kanda yenye mizozo ya mashariki ya kati. Mara nyingi alichukua jukumu la mpatanishi katika mazungumzo kati ya wahasimu wawili wakuu Iran na Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG