Watunisia wameshiriki katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais hii leo, kumchagua kati ya msomo mhafidhina Kais Saied, na mfanya biashara tajiri mmiliki vyombo vya habari Nabil Karoui, aliyeachiliwa huru siku ya Jumatano.
Karoui aliachiliwa huru baada ya kuwekwa kizuizini kwa muda wa mwezi mmoja kwa tuhuma za kurudisha katika utaratibu wa haliali fedha alizopata kwa njia haramu, na hakuweza kufanya kampeni zake kwa njia huru.
Wagombea hao wawili wepya katika siasa za Tunisia waliwashinda wanasiasa wa muda mrefu na walokuwa madarakani katika duru ya kwanza.
Hii ni kutokana na hasira za wananchi kwa kuduma kwa uchumi, ukosefu wa ajira na huduma dhaifu ya uma pamoja na wapiga kura kuchoshwa na wanasiasa wa kawaida wanaolumbana kila wakati.
Uchaguzi huu wa pili huru wa rais tangu mapinduzi ya wananchi ya 2011, unafanyika kufuatia kifo cha Rais Beji Caid Essebsi mwezi wa Julai.
Uchunguzi wa maoni wakati wa kupiga kura unaonesha wapiga kura wamegawika kati ya wagombea hao wawili mmoja wakjisewma atatekeleza sheria na wapili anaewasaidia maskini.
Hapo wachambuzi wanaeleza kwamba mgombea anaewasaidia maskini ni tajiri Karoui aliyepata umaaufu kutokana na kipindi chake cha televisheni cha hisani kinachowasaidia maskini.
Na mgombea ambae huwenda akatekeleza sheria ni Mhadhiri wa sheria mtaalamu wa masuala ya katiba Saied aliyeshinda katika duru ya kwanza lakini hakupata zaidi ya asili mia 50 kushinda moja kwa moja.
Mfanyabishara Karoui anadai yeye ni mpinzani mkubwa wa siasa za kislamu anamtuhumu mpinzani wake Said kuwa ni mungaji mkono wa siasa hizo.
Vituo vya kupiga kura vilifungwa saa kumi na mbili saa za Tunisia na matokeo ya awali yataweza kujulikana baadae hii Jumapili na matokeo rasmi yatatangazwa Jumanne.