Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 02, 2021 Local time: 21:48

Kampuni ya madini huko Morocco imepata shehena yake ya dhahabu iliyozuiliwa Sudan


Mfano wa shehena ya dhahabu ziizozuiliwa Sudan mali ya kampuni ya MANAGEM

MANAGEM inazalisha dhahabu, fedha, kobalti na shaba. Kampuni hiyo pia inaendesha shughuli zake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Ethiopia, Gabon, Guinea Conakry, ivory Coast, mali, Morocco na Sudan

Kampuni kuu ya madini ya Morocco ya MANAGEM ilieleza Jumanne kwamba imepata shehena ya dhahabu ambayo ilizuiwa na maafisa wa Sudan mwanzoni mwa mwezi huu.

Kikosi cha kukabiliana na mambo ya dharura nchini Sudan kilizuia kilo 241 za dhahabu katika ndege ambayo ilitua mjini Khartoum Mei 8 wakati kikosi hicho kililipokua kinafanya uchunguzi unaohusisha uwezekano wa kuwepo na usafirshaji haramu wa dhahabu.

MANAGEM ilieleza kuwa shehena hiyo ni sehemu ya usafirishaji wa kawaida na kampuni ilikamilisha utaratibu wote unaohitajika kulingana na kanuni za mamlaka ya usafiri ya nchi hiyo. MANAGEM iliendelea kueleza katika taarifa yake kwamba maafisa wa mji mkuu wa Sudan walikubali utaratibu tunaofuata na kuheshimu kanuni zilizopo nchini humo huku ikiongeza kwamba ndege hiyo hivi sasa iliruhusiwa kuendelea na safari.

Kipande cha dhahabu
Kipande cha dhahabu

Kampuni ya MANAGEM ambayo inamilikiwa na kampuni ya familia ya kifalme ya Morocco ya Almada iliyoanzisha uzalishaji wa mgodi wa dhahabu wa Gabgaba mwaka 2012 kupitia kampuni yake tanzu ya MANUB. MANAGEM inazalisha dhahabu, fedha, kobalti na shaba. Kampuni hiyo pia inaendesha shughuli zake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Ethiopia, Gabon, Guinea Conakry, ivory Coast, mali, Morocco na Sudan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG