Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 14:44

Kayihura aachiliwa kwa dhamana


General Kale Kayihura
General Kale Kayihura

Aliyekuwa mkuu wa polisi nchini Uganda Genereali Edward Kale Kayihura, Jumanne aliachiliwa kwa dhamana na mahakama ya kijeshi baada ya kuzuiliwa kwa muda wa takriban miezi mitatu.

Kayihura hata hivyo haruhusiwi kusafiri nje ya jiji la Kampala wala nje ya nchi, na anatakiwa kuripoti kwa mahakama ya kijeshi kila siku ya jumatatu ya kila mwanzo wa mwezi hadi kesi inayomkabili ya kushindwa kulinda sialaha na utekaji nyara itakapokamilika.

Generali Kayihura amekuwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi katika kambi ya Makindye jijini Kampala, na hatimaye alipata uhuru wa mda lakini chini ya masharti na uangalizi mkali kutoka kwa magenerali wenzake.

Dhamana

Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 zisizo pesa taslimu baada ya majenerali wenzake wakiwemo generali Sam Kavuma, meja generali James Mugira kudhamini huru wake wenye masharti, kwa kiasi cha shilingi milioni 5 zisizo pesa taslimu.

Katika kuomba kuachiliwa kwa dhamana, Kayihura alieleza mahakama ikiongozwa na Jaji generali Andrew Gutti, kwamba alihitaji kuwa huru ili asafiri na kupokea matibabu jijini Nairobi Kenya.

Aidha alisema umri wake hauwezi kumruhusu kusalia kizuizini na kwamba kuachiliwa kwa dhamana ni haki ya kikatiba, hoja ambazo mahakama ya kijeshi iliridhia, licha ya kwamba mashtaka yanayomwandama mshukiwa huyo ni mazito na ambayo adhabu yake ni kifo.

Mashtaka yanayomkabidhi

Kayihura, ambaye katika utawala wake kama mkuu wa polisi alisema mara kadhaa kwamba anafanya kazi yake kwa kufuata masharti ya rais Museveni, anakabiliwa na mashtaka ya kushindwa kulinda silaha zikiwemo bunduki na risasi, kuwateka nyara wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Kuwarudisha kwao kinyume na sheria.

Kati ya wakimbizi hao ni aliyekuwa mlinzi wa rais wa Rwanda Paul Kagame Lt Joel Mutabazi, aliyetekwa nyara na maafisa wa ngazi ya juu katika polisi wa Uganda na kurejeshwa Rwanda mnamo mwaka 2012 kabla ya kufunguliwa mashtaka ya kuhatarisha usalama wa Rwanda.

Kashafa wakati wa uongozi wake

Utawala wa Kayihura uligubikwa na matumizi ya nguvu hasa dhidi ya wakosoaji wa rais Museveni, akitumia viboko, gesi ya kutoa machozi, pilipili na risasi kutawanya na kukamata wapinzani wa Museveni.

Utawala wake vile vile ulishuhudia wanasiasa wa upinzani kuzuiliwa nyumbani kwao, vifo vya watu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana na utekaji nyara wa raia, akishutumiwa kuwapa silaha makundi ya vijana wakiwemo kundi la wahudumu wa bodaboda 2010 wakiongozwa na Abdalla Kitatta ambaye pia anazuiliwa katika gereza la kijeshi jijini Kampala. Hata hivyo, fumbo ambalo limewashinda waendesha mashtaka ni kujua aliyemuua naibu wa Kayihura, Afelix Kaweesi

Bobi Wine

Wakati huo huo, mbunge Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, amelazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Rubaga jijini Kampala akiuguza majeraha yaliyotokana na kupigwa na walinzi wa rais Yoweri Museveni SFC.

Spika aandikia Museveni

Spika wa bunge Rebecca Kadaaga, alimwandikia rais Museveni barua, akitaka walinzi wa rais SFC, waliohusika katika kuwapiga wabunge, raia na waandishi wa habari, wakamatwe na kushitakiwa katika kipindi cha siku mbili kinachokamilika kesho jumatano, la sivyo aanze mkomo wa kuongoza shughuli za bunge.

Imetayarishwa na: Kennes Bwire, Washington DC

XS
SM
MD
LG