Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:52

Katumbi akataliwa kuingia Kongo na maafisa wa uhamiaji


Kiongozi wa upionzani wa DRC Moïse Katumbi katikati ya wafuasi wake alipowasili mji wa mpakani wa Kasumbalesa hapo Ogusti 3 2018. (Facebook/Katumbistes Congolais)
Kiongozi wa upionzani wa DRC Moïse Katumbi katikati ya wafuasi wake alipowasili mji wa mpakani wa Kasumbalesa hapo Ogusti 3 2018. (Facebook/Katumbistes Congolais)

Kiongozi mashuhuri wa upinzani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo akataliwa ruhsa ya kuingia nchini baada ya kufika katika ofisi ya uhamiaji katika mji wa mpakani wa Kasumbalesa.

Moise Katumbi Chapwe mpinzani mkubwa wa RaisJoseph Kabila aliwasili katika ofisi ya uhamiaji ya Kongo mjini Kasumbalesa na kuhojiwa na maafisa wa uhamiaji baada ya kuwasilisha rasmi maombi ya kurudi nyumbani.

Mwandishi wa Sasuti ya Amerika mjini Lumbumbashi, Kahozi Kosha, anaripoti kwamba baada ya kuhojiwa maafisa waliondoka na na kumacha Katumbi ndani ya ofisi hiyo bila ya kumpa taarifa yeyote.

Muda mfupi baadae aliamua kurudi Ndola, Zambia mahala alikofikia siku ya Ijuma baada ya ndege yake kutoruhusiwa kutua Lumbumbashi.

Haifahamiki ni hatua gani atakazochukua kwa hivi sasa lakini anasema anataka kuhakikisha anaingia nchini kufuatana na sheria,akisema atapigana dhidi ya uwamujzi wa kukataliwa kurudi nyumbani.

Katumbi anatarajia kujiandikisha katikatume ya uchaguzi kabla ya siku ya mwisho ya Ogusti 8 kuweza kushirikikatika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG