Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 16, 2022 Local time: 01:18

Mwandishi wa 'Mwananchi' hajulikani alipo Tanzania


Ukurasa wa gazeti la Mwananchi

Kampuni ya magazeti ya Mwananchi inatowa wito kwa mamlaka ya usalama kuwasaidia kumtafuta au kutoa habari kuhusu kutoweka kwa mwandishi wao Azory Gwanda.

Mkurugenzi mtendaji wa Mwananchi, Francis Nanai akizungumza na Sauti ya Amerika anasema wametoa taarifa Jumatatu baada ya kupokea habari kutoka kwa familia yake kwamba Gwanda ametoweka tangu Novemba 21 mjini Kibiti karibu na Dar es Salaam.

Nanai anasema kwa vile ni mwandishi wa kujitegemea hajakuwa na mawasiliano ya kila siku na kampuni isipokuwa wakati kuna habari muhimu ya kuripoti na hivyo hakuna mawasiliano ya siku hadi siku na Gwanda.

Francis Nanai mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mwananchi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00

Anasema mara ya mwisho kuwasiliana na mwandishi huyo wa Mwananchi ilikuwa Novemba 20 na tangu wakati huo hapatikani kwenye simu zake tatu.

Gwanda mwenye umri wa miaka 42 amekua akiandika mfululizo wa ripoti juu ya kutoweka kwa raia na maafisa wa usalama katika mji wa Kibiti, na haifahamiki ikiwa hiyo ndio sababu ya kutekwa kwake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG