Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 21:24

Harakati za kijeshi zaleta wasiwasi Harare


Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantine Chiwenga, akimpongeza Rais Robert Mugabe wakati wa kuapishwa kwake 2008.

Hali ya wasiwasi imeingia katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, ikiwa ni pamoja na kuonekana kwa vifaru vinne vikielekea katika mji mkuu huo kulingana na mashahidi, siku moja baada ya mkuu wa majeshi Jenerali Constantino Chiwenga kumuonya Rais Robert Mugabe kutoendelea na mpango wa kuwaondowa mashujaa wa vita kutoka chama tawala.

Jenerali Chiwenga amesema "ni lazima ni wakumbushe wanaozusha mvutano wa hivi sasa wa kisiasa kwamba, inapohusiana na kulinda mapinduzi yetu, jeshi halitosita kuingilia kati".

Rais Robert Mugabe akizungumza na mkuu wa majeshi Jenerali Constantino Chiwenga mjini Harare, Zimbabwe.
Rais Robert Mugabe akizungumza na mkuu wa majeshi Jenerali Constantino Chiwenga mjini Harare, Zimbabwe.

Mapema Jumanne Chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe MDC kilitowa wito wa kulinda utawala wa kiraia. Waziri kivuli wa masuala ya kijeshi wa MDC Gift Chimanikire amesema kwamba "hakuna mtu anaetaka kushuhudia mapinduzi, sidhani kuna jaribio la mapinduzi lakini ikiwa jeshi litachukua madaraka hilo sijambo linalotarajiwa kwani hatua hiyo itafikisha kikomo demokrasia nchini mwetu".

Kwa upande wake tawi la vijana la chama tawala cha ZANU-PF kinachomunga mkono Grace limetowa taarifa Jumanne kusema kwamba mkuu wa jeshi Chinwenga hatoruhusiwa kuteuwa viongozi wa Zimbabwe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG