Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:46

Mvutano ndani ya chama cha Republican Marekani


Sen Jeff Flake, wa Arizona akifuatna na mkewe Cheryl wakiondoka bungeni, Washington Jumanne, Oct 24 2017, baada ya kutangaza hatogombania tena kiti chake.
Sen Jeff Flake, wa Arizona akifuatna na mkewe Cheryl wakiondoka bungeni, Washington Jumanne, Oct 24 2017, baada ya kutangaza hatogombania tena kiti chake.

Rais Donald Trump wa Marekani alitembelea bunge Jumanne mchana ili kukutana na viongozi wa chama chake cha republican kujaribu kupunguza mvutano unaojitokeza hadharani katika chama hicho tawala, pamoja na kuhamasisha mpango wake wa kupunguza kodi.

Mpasuko mpya wa ghafla ulitokea siku hiyo ya Jumanne pale seneta wa Arizona, Jeff Flake alishambulia vikali tabia ya rais, alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Senate na kutangaza kwamba hatagombania tena kiti chake katika uchaguzi wa mwakani.

Flake ambae ni Seneta anaekamilisha mhula wake wa kwanza baada ya kuwa mbunge kwa miaka 12 katika Baraza la Wawakilishi, alisema, "ni jambo lisilokubalika kukaa kimya wakati maadili na thamini inayoifanya Marekani kuwa thabiti inahujumiwa na wakati ushirika na mikataba inayohakikisha utulivu duniani kote daima iko hatarini kutokana na maandishi ya herufi 140." Akizungumzia ujumbe wa Twitter wa Trump.

Flake ansema "chama cha Republican kimejidanganya kwa muda mrefu kwamba Trump atabadilika na kuwa muadilifu."

Sen. Jeff Flake, R-Ariz., katikati, akielekea kukaa katika chakula cha mchana bungeni na Rais Donald Trump
Sen. Jeff Flake, R-Ariz., katikati, akielekea kukaa katika chakula cha mchana bungeni na Rais Donald Trump

Mashambulio hayo makali amabyo si kawaida kufanywa na seneta dhidi ya rais kutoka chama chake yametokea saa chache tu baada ya Trump kugombana na seneta mwengine wa chama cha Republican Bob Corker wa Tennessee.

Corker ambae pia ameamua kutogombania tena kiti chake baada ya kutumikia jimbo lake kwa miongo kadhaa, amesema washauri wa ikulu walimuomba kuingilia kati wakati Trump, “anakaribia kufanya jambo ambalo haliambatani kamwe na ukweli wa mambo.”

Corker anasema, “mtu mwenye akili ya namna hiu kuwa rais wa Marekani ni jambo ambalo ninadhani inashusha hadhi ya nchi yetu.”

XS
SM
MD
LG