Upatikanaji viungo

Breaking News

Jeshi la Kenya lashutumiwa kwa mauaji ya kiholela


Gari la jeshi la Kenya, KDF. Vikosi vya jeshi la Kenya vimeshutumiwa kwamba viliwaua kiholela watu watano ambao walikuwa wameripotiwa kupotea katika kaunti ya Mandera. Miili yao hatimaye ilipatikana imezikwa kwenye kaburi la kina kifupi.

Maafisa wa kaunti ya Mandera nchini Kenya, siku ya Jumanne walilishutumu jeshi la nchi hiyo kwamba liliwaua watu watano ambao walikuwa wamepotea, na miili yao kupatikana kwenye kaburi lisilo na kina kirefu.

Akizungumza wakati wa mazishi ya watu hao watano ambao miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu, naibu gavana wa kaunti hiyo, Omar Maalim, alidai kwamba mashirika ya serikali yalihusika kwa vifo vyao kama njia mojawapo ya kupambana na itikadi kali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, AP, naibu gavana alisema kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na vikosi vya jeshi la Kenya, KDF.

“Tuna habari kwamba watu hawa watano walichukuliwa na jeshi kutoka manyumbani mwao, na kushikiliwa kwa muda mfupi katika kituo cha polisi cha Finno," alisema Maalim.

Kamishna wa kaunti hiyo, Fredrick Shisia, alithibitisha kwa njia ya simu kwamba watano hao walikuwa kati ya watu 11 waliokuwa wamekamatwa.Ijumaa usiku.

AP hata hivyo iliripoti kwamba maafisa wa usalama wa serikali ya Kenya hawakupatikana ili kutoa kauli kuhusiana na tuhuma hizo.

  • 16x9 Image

    BMJ Muriithi

    BMJ Muriithi is an international Broadcaster/ Multimedia specialist with Voice of America (VOA) and is based in Washington DC. He previously worked as a stringer, filing stories from Atlanta, Georgia, as well as the international correspondent for Nation Media Group, Kenya. He is a versatile journalist who has widely covered international affairs, including on-location reports of UN summits in New York and AU deliberations in Addis Ababa, Ethiopia. He also reports on regular day-to-day happenings and human interest stories from around the world.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG