Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:51

UM: 'Uchunguzi wa matumizi ya kemikali Mosul ufanyike '


Familia huko Iraqi zakimbia kutoka Mosul kufuatia mashambulizi ya kikundi cha Islamic State
Familia huko Iraqi zakimbia kutoka Mosul kufuatia mashambulizi ya kikundi cha Islamic State

Mratibu wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa huko Iraq ametoa tahadhari juu ya uwezekano wa kutumika silaha za kemikali huko Mosul, ambako wapiganaji wa Islamic State wanapambana na wanajeshi wa Iraq wanaosaidiwa na Marekani.

Hili ni jambo la kutisha, amesema Lise Grande, Naibu mwakilishi maalum wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, na ametaka mara moja uchunguzi ufanyike.

Amesema iwapo madai ya matumizi ya silaha za kemikali zitathibitishwa , itakuwa ni uvunjaji wa sheria za haki za kibindamu za kimataifa na uhalifu wa kivita, bila ya kujali nani walioshambuliwa au ni nani wahanga wa mashambulizi hayo.”

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kimataifa (ICRC) limesema kuwa watu saba wamelazwa katika hospitali karibu na Mosul na wanatibiwa kutokana na kile kinacho dhaniwa kuwa ni athari za mashambulizi ya silaha za kemikali.

Robert Mardini, Mkurugenzi wa eneo la Mashariki ya Kati was ICRC, amesema kuwa watoto watano na wanawake wawili wanaotibiwa katika hospitali wameonyesha dalili za uchunguzi za tiba zinazolingana na athari za kemikali zilizojitokeza katika ngozi zao.

“Dalili hizo ni pamoja na kubanduka ngozi, macho kuwa mekundu, kuwashwa, kutapika na kukohoa. Hata hivyo utumiaji wa silaha za kemikali ni kitendo kilichopigwa marufuku kabisa chini ya sheria za kibinadamu za kimatiafa,” Mardini amesema.

“Tumeshtushwa sana na kile ambacho wenzetu wamekiona na tunalaani vikali matumizi yoyote ya silaha za kikemikali, kutoka upande wowote na mahali popote,” amesema.

Madai ya mashambulizi hayo yameripotiwa tangia wiki iliyopita huko Mashariki ya Mosul.

XS
SM
MD
LG