Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:14

Wajumbe wa UN watembelea nchi nne Afrika Magharibi


Watoto wasimama mlangoni kibanda kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya nchi nchini Nigeria Nov. 29, 2016.
Watoto wasimama mlangoni kibanda kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya nchi nchini Nigeria Nov. 29, 2016.

Wanadiplomasia wa baraza la usalama la umoja wa mataifa Jumatano walianza safari ya kwelekea bonde la ziwa Chad, huko Afrika Magharibi, kujionea wenyewe changamoto za kiusalama na hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo.

Mabalozi kutoka nchi 15 wanachama wa chombo hicho kilicho na nguvu Zaidi kwenye umoja wa mataifa, watatembelea nchi za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria, katika ziara hiyo ya siku nne.

Hii ni mara ya kwanza kwa baraza hilo kutembelea bonde hilo la ziwa Chad.

Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa, na ambaye ni rais wa baraza hilo, Matthew Rycroft, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba wanafahamu kuwa kuna tishio la usalama wa kimataifa katika nchi hizo nne, akimaanisha uwepo wa kundi la kigaiodi loa Boko Haram katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG