Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:49

Mugabe asema hatomteua mtu kuchukua nafasi yake


Rais Mugabe akihutubia maelfu ya wafuasi siku ya kuzalkiwa kwake
Rais Mugabe akihutubia maelfu ya wafuasi siku ya kuzalkiwa kwake

Kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe, Rais Robert Mugabe amesema, "sitolazimisha kuteuliwa mtu kuchukua nafasi yangu na chama kikihisi inabidi mimi nistahafu, basi kiitishe mkutano mkuu kumchagua kiongozi mpya".

Kiongozi huyo mzee kabisa duniani alitimia umri wa miaka 93 siku ya Jumanne, na amekua madarakani kwa kwa zaidi ya miaka 40, tangu Zimbabwe kupata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1980.

Keki ya kuadhimisha siku ya kuzalikwa Rais Robert Mugabe ...
Keki ya kuadhimisha siku ya kuzalikwa Rais Robert Mugabe ...

Mugabe aliungwa mkono na maelfu ya wafuasi wake kusherekea siku ya kuzaliwa kwake katika shule ya Matobo nje kidogo ya mji wa pili kwa ukubwa wa Bulawayo. Wakosowaji wamelaani gharama kubwa ya kuanda sherehe hizo wakati nchi inakabiliwa na hali mbaya ya ucuhumi.

Rais Mugabe anasema ameweza kuishi maisha marefu kutokana na "matakwa ya Mola kunitaka kutekeleza mahitaji ya wa-Zimbabwe."

Katika hotuba yake ya karibu saa moja kiongozi huyo aliyeonekana mdhaifu alimshukuru mwenyezi mungu kwa kumpa maisha marefu na muda mwingi kuzungumzia maisha yake mwenyewe.

XS
SM
MD
LG