Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 13:00

Kundi la Sinared Lashinikiza Serikali ya Burundi Ikutane Nao Ana Kwa Ana


Rais mstaafu Benjamin Mkapa

Rais mstaafu Benjamin Mkapa ameeleza kuwa ameridhishwa na mwitikio wa wajumbe waliohudhuria katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, akisema yamempa matumaini.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa licha ya mazungumzo kufanyika katika jengo moja wakati wote huo kundi la Sinared halikuweza kukaa kwenye meza ya mazungumzo.

Kundi hilo pia halikushiriki pamoja na makundi mengine kwa madai kuwa wao wanataka kuonana na wawakilishi wa serikali ambao nao hawakuwa tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kundi hilo.

Hata hivyo Mkapa ambaye ndiye msuluhishi mkuu ameeleza kuwa baada ya kusikiliza hoja za wajumbe hatua itakayofuata ni kuangalia uwezekano wa kukutana na mwenyekiti wa kusuluhisha mgogoro huo na mwenyekiti wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa siku tatu ulimalizika Jumapili huko Arusha, Tanzania.

Msimamizi huyo amesema kinachotia moyo ni kuona asilimia kubwa ya wajumbe wa pande zote wanakubaliana na masuala muhimu yanayogusa maisha ya wananchi wa Burundi.

Ameongeza kuwa pia wanakubaliana na mapendekezo yaliyotolewa ya kuhakikisha kuwa suala la utulivu wa kisiasa, ustawi wa kiuchumu, na mahusiano ya burundi na nchi nyingine yanapewa kipaumbele.

Wakizungumza baada ya kumalizika kwa kikao hicho katibu mkuu wa chama tawala cha (CNDD -FDD ) Evariste Ndayishimiye na kiongozi wa kundi la Sinared, ambao ni wapinzani wakubwa wa serikali, Jean Minan na baadhi ya wajumbe wote kwa pamoja wamekiri kuwa hatua iliyofikiwa inaleta matumaini ingawaje wameendelea kutofautiana huku kila mmoja akishikilia msimamo wake.

XS
SM
MD
LG