Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 16:49

Chama Tawala Burundi Chasisitiza Kuwa Kuna Amani na Usalama Burundi


General Evariste Ndayishimiye

Kiongozi wa chama Tawala cha CNDD FDD nchini Burundi, Evariste Ndayishimiye amewataka wananchi wa nchi hiyo waliokimbilia nchi jirani kurejea Nyumbani.

Akizungumza nje ya ukimbi yanakofanyika mazungumzo hayo Evariste Ndayishimiye amesema wananchi wengi waliokimbia kutokana na hofu iliosambazwa na baadhi ya wanasiasa, wafahamu kuwa Burundi kuna amani na usalama wa kutosha.

Mazungumzo ya amani ya mgogoro wa Burundi ambayo yanasimamiwa na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa yanaendelea mjini Arusha, Ijumaa yakiwa katika siku yake ya pili na yamehudhuriwa na vyama mbalimbali vya kisiasa kutoka Burundi.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa suala la kutokuwepo kwa wawakilishi wa serikali katika meza ya mazungumzo sio tatizo kabisa. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kumalizika Jumamosi.

Rais Mkapa ambae ni msuluhishi wa mgogoro huo benjamini mkapa alisema kuwa hilo sio tatizo.

Msuluhishi huyo amesema kuwa hata yeye haoni sababu ya baadhi ya wajumbe kuwa na wasiwasi juu ya kutokuwepo kwa wawakilishi wa serikali kwani hoja ambazo zimewasilishwa na chama tawala ndio hizo hizo ambazo zingewasilishwa na serikali.

Kwa upande wake msemaji wa Naibu Spika wa Bunge la Burundi Bw Aime Magera amesema hofu ya wananchi waliokimbilia nchi jirani juu ya usalama wao haipaswi kupuuzwa.

Imetayarishwa na Mwandishi wa wetu, Tanzania

XS
SM
MD
LG