Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:03

Trump amtetea Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa taifa


MAKTABA: Rais Donald Trump na Luteni Jenerali mstaafu Michael Flynn wanaonekana kwenye picha hii wakiwa mjini Palm Beach, Florida.
MAKTABA: Rais Donald Trump na Luteni Jenerali mstaafu Michael Flynn wanaonekana kwenye picha hii wakiwa mjini Palm Beach, Florida.

Rais Donald Trump, Jumatano alimtetea aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa taifa, Michael Flynn, ambaye alimfukuza kazi siku ya Jumatatu, na kusema kuwa afisa huyo aliathiriwa na uvujaji wa siri kutoka kwa jamii ya kijasusi ya Marekani, zilizokuwa na maelezo kuhusu mazungumzo kati yake na balozi wa Russia mjini Washington.

Trump aliongeza kuwa Flynn alitendewa vibaya mno na vyombo vya habari.

Hata hivyo, rais Trump, aliyekuwa akiwahutubia waandishi wa habari katika ikulu, huku akiandamana na waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, hakuelezea na kwa nini alimlazimisha Flynn kujiuzulu, baada ya kufanya kazi kwa siku 24 tu.

“Nadhani ni jambo la kuhuzunisha kuwa Flynn alitendewa vibaya hivyo,” alisema Trump, na kuongeza kuwa nyaraka za siri zinaendelea vuja kutoka idara za kuijasusi. Rais huyo alisema kuwa uvujaji huo umeongezeka mno, na kwamba ulikuwa ukiendelea hata kabla yake kuingia mamlakani. Alisema hicho ni kitendo cha uhalifu.

Siku ya Jumanne, msemaji wa ikulu Sean Spicer, alisema kuwa imani ya rais Trump kwake Flynn, ilikuwan imepungua.

XS
SM
MD
LG