Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:55

Trump, Netanyahu kukutana Washington DC


Rais Donald Trump alitarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, mjini Washington DC siku ya Jumatano Februari 15, 2017.
Rais Donald Trump alitarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, mjini Washington DC siku ya Jumatano Februari 15, 2017.

Huku rais Donald Trump akijitayarisha kufanya mkutano wake wa kwanza akiwa rais na Waziri mkuu wa Isreaeli, Benjamin Netanyahu, wachambuzi wanasema kuwa kiongozi huyo wa Israeli anatumai kuwa atamshawishi mwenyeji wake kumuunga mkono katika msimamo wake kuhusu ya maswala ya Iran na yale ya kieneo.

Netanyahu, ambaye alitarajiwa kuzuru Marekani Jumatano, atakuwa kiongozi wa nne wa nchi ya kigeni, kukutana ana kwa ana na Trump katika ikulu.

Waliomtangulia ni Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau.

Waziri mmoja wa ngazi za juu nchini Israeli, alisema siku ya Jumatatu kuwa Netanyahu hatambui Palestina kama taifa huru, lakini hakusema kama waziri huyo mkuu angeyasema hayo wazi wazi wakati wa mkutano na rais Trump baadaye Jumatano.

XS
SM
MD
LG