Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 06:18

Rais Magufuli amteua Mkuu wa Majeshi mpya


Rais Magufuli pamoja na viongozi wa Jeshi na polisi Ikulu
Rais Magufuli pamoja na viongozi wa Jeshi na polisi Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Tanzania.

Pamoja na uteuzi huo mkuu wa majeshi huyo amepandishwa cheo kuwa Jenerali.

Jenerali Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Akizungumzia uteuzi wa maafisa wakuu walioteuliwa na kuapishwa Januari 30 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amesema ni pamoja na Meja Jenerali James Mwakibolwa ambaye amekuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi kavu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenarali Salum Mustafa Kijuu, Meja Jenerali Yakub Sirakwi anakuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gaudence Milanzi ambaye amateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

XS
SM
MD
LG