Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 16:52

UNHCR: Wakimbizi sio hatari kwa usalama wa Marekani


Wakimbizi wa Syria
Wakimbizi wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa wakimbizi kutoka Syria na wengine hawahatarishi usalama wa Marekani.

Shirika hilo limesema kuwa hakuna uthibitisho katika madai ya Rais Donald Trump kwamba wakimbizi wa Syria wanahatarisha usalama wa taifa na hivyo ni lazima waruhusiwe kuingia Marekani.

Siku ya Ijumaa, Rais Trump alisaini amri ya rais ikipiga mrufuku raia wanaotoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani kwa kipindi cha siku 90.

Sera hiyo mpya pia inataka kusimamishwa kwa siku 120 utaratibu wote wa kuwapokea wakimbizi nchini na kuwapa makazi na kupiga marufuku kabisa wakimbizi wa Syria kuingia Marekani.

Msemaji wa UNHCR Vannina Maestracci amepinga kauli inayosema kuwa wakimbizi wa Syria ni magaidi. Amesema wakimbizi ni waathirika wa ugaidi na wale waliopendekezwa kutafutiwa makazi ni kati ya watu ambao maisha yao yako hatarini kweli kweli. Kati yao wako wanawake, watoto, watu walemavu na wenye kuhitaji matibabu haraka sana.

Ameiambia VOA kuwa wakimbizi wanapitia katika machakato wa usaili wa kina kabla ya kukubaliwa kuingia Marekani kwa ajili ya kupatiwa makazi..

“Nafikiri ni sawa kusema kuwa wakimbizi wanaokuja Marekani wakitafuta makazi ni ya wale wenye kufanyiwa usaili wa kina zaidi kati ya watu wanaoingia Marekani,” amesema msemaji huyo.

XS
SM
MD
LG