Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:10

Mahakama yazuia amri ya kiutendaji ya Trump inayowabana wahamiaji


Waandamanaji wakusanyika uwanja wa kimataifa wa John F. Kennedy huko New York kupinga amri za kiuetendaji zinazowazuia wahamiaji.
Waandamanaji wakusanyika uwanja wa kimataifa wa John F. Kennedy huko New York kupinga amri za kiuetendaji zinazowazuia wahamiaji.

Jaji wa serikali kuu huko New York, Jumamosi usiku, amesitisha kwa muda amri ya kiutendaji iliyotolewa na Trump inayowataka wahamiaji kutoka baadhi ya nchi za Kiislamu warejeshwe makwao baada ya kuwasili nchini Marekani pamoja nakuwa na viza halali.

Hata hivyo, masaa baada ya kutolewa amri hiyo iliyosainiwa na Trump, waandamanaji wakipinga kadhia hiyo wamekusanyika katika viwanja vya ndege na mawakili wamesema kuwa wateja wao wamekwama nje ya Marekani au wamezuiliwa katika viwanja vya ndege.

Amri ya kupiga marufuku wahamiaji ilianza kutumika Ijumaa usiku, ikieneza hofu kubwa na watu kuchanganyikiwa, wakati maafisa wa serikali wakiangalia namna ya kuitekeleza.

Amri ya kiutendaji aliosaini Rais Trump inayozuia baadhi ya wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani zimepelekea kuwachanganya wahamiaji.

Kati ya wahamiaji hao kuna wenye green-card, wanafunzi na wafanyakazi wenye visa ambao wamezuiliwa katika baadhi ya viwanja vya ndege au wamekataliwa kupanda ndege za kimataifa Jumamosi.

Trump alisema mapema Jumamosi kuwa amri hiyo mpya ya kuwazuia wahamiaji kutoka baadhi ya nchi kuingia Marekani “imefanya kazi vizuri sana kabisa. Unaishuhudia katika viwanja vya ndege, unaiona kila pahali.”

Trump ameongeza, “sisi tutakuwa na amri kali sana itayozuia wahamiaji, na tutakuwa na uchunguzi wa kina, kitu ambacho tulipaswa kuwa nacho miaka mingi nyuma.”

Hii inamaanisha “uchunguzi wa kina” anaokusudia Trump unahusiana na mpango wake wa kuwasaili kwa kina Waislam na watu wengine ambao wanadhaniwa kuwa ni hatari kwa Marekani kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini.

Wakati huo huo, amri hiyo imekutana na kizingiti cha kisheria cha kwanza, changamoto ya kisheria ambayo imeletwa na watu wawili waliozuiliwa katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy huko Jijini New York. Umoja wa Uhuru wa Wananchi wa Marekani unaongoza katika kupambana na changamoto hiyo ya kisheria, ikisaidiwa na makundi mengine ya utetezi.

Mpaka Jumamosi jioni, maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika viwanja vya ndege katika miji mikubwa kupinga amri ya kiutendaji, iliyoongeza mkanganyiko wa amri hiyo.

Wabunge wa Marekani wanaendelea kutoa maoni yao ambapo kati yao wako wanaokubaliana na amri ya kiutendaji na wengine wakiikataa.


XS
SM
MD
LG