Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:55

Mahakama Kenya yaamuru Wasudani 2 wasirejeshwe makwao


Mahaboub Maali, Kiongozi wa mazungumzo ya kambi ya upinzani ya Sudan Kusini
Mahaboub Maali, Kiongozi wa mazungumzo ya kambi ya upinzani ya Sudan Kusini

Mahakama nchini Kenya imetoa amri kuwa raia wawili wa Sudan Kusini ambao hawajulikani waliko tangu Jumatatu wasirejeshwe makwao.

Hakimu Luka Kimaru alitoa uamuzi huo baada ya mawakili wa familia ya Samuel Dong na Aggrey Idris walipofungua mashtaka dhidi ya serikali wakitaka serikali ielezee mahali waliko raia wawili hao.

Uchunguzi juu ya kutoweka Wasudani

Hakimu Kimaru amemwamuru Afisa wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai katika Kaunti ya Nairobi, Nicholas Kamwende kuanzisha uchunguzi juu ya kutoweka kwa raia hao na kukabidhi ripoti hiyo mahakamani Jumanne ijayo.

Pia Kimaru ameagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa usalama katika Serikali ya Sudan Kusini aliyeko nchini ilikufahamu iwapo anahusika na kutoweka kwa watu wawili hao.

Aidha, Mahakama imeagiza makampuni ya simu nchini kufikisha mahakamani maelezo muhimu ya mawasiliano kuhusu Idris na Dong.

Imeandaliwa na mwandishi wa VOA Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG