Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 05:43

Rais Museveni awashukia wale wanaobeza utawala wake Uganda


Rais Yoweri Kaguta Museveni

Rais amesema hayo wakati wa kuadhimisha miaka 31 ya utawala wake Alhamisi akiongezea kuwa yeye ni mpiganiaji uhuru ambaye pia anapigania nafsi yake.

"Mnadhani mimi ni mtumishi wenu, hapana mimi ni mpingania uhuru tu ambaye napigania nafsi yangu," amesema Museveni.

Ameongeza kusema: "Wale wanaodhani mimi ni mjinga basi watakutana na hasira za huyo mtu wanayemdhania hivyo."

Wachambuzi wa siasa wamesema kuwa usemi wake Museveni kwamba yeye si mtumishi, ni kinyume na ule wa viongozi wenzake kama vile Dkt Magufuli ambaye siku zote amekuwa akisema amejitolea sadaka kwa watanzania.

Kadhalika mfano mwengine wa kiongozi ambaye ameendelea kuliambia taifa yeye ni mwajiriwa ni uhuru Kenyatta wa Kenya na kuwaita wakenya ndio waajiri wake.

Pia wachambuzi wametoa mfano wa Paul Kagame ambaye amekuwa akisema kuwa anaheshimu maamuzi na sauti za raia wa Rwanda.

Museeveni pia ametangaza kuchukua maamuzi magumu ya kubana matumizi katika serikali yake.

Amesema atafanya hivyo ilikuhakikisha kuwa Uganda inastawi kwa hararaka na kuacha kutegemea ufadhili wa nchi zilizoendelea.

anaripoti kuwa Rais Museveni alikuwa akitumia lugha yake Kinyankole na kiingereza, wakati analihutubia taifa.

Museveni ametangaza kuchukua maamuzi magumu ya kubana matumizi ya fedha za serikali ikiwa pamoja na kupunguza bajeti ya kila wizara kwa asilimia 10.

Safari kwa mawaziri wake na watumishi wengine wa uma nazo ametangaza kupunguzwa katika hatua anayosema itasaidia kuekeza pesa zaidi katika sekta zitakazowezesha Uganda kutajirika.

Museveni ameeleza kukasirishwa na nchi alizotaja kuwa kubwa duniani, kumnyima mikopo kila mara, akisema atakapoanza kuchimba mafuta yake, hataomba msaada kutoka kwa nchi yoyote na kutaka wananchi wake kuanza mikakati ya kujitosheleza kwa kuzalisha bidhaa zao wenyewe.

“Mnanununua kila kitu kutoka china. Nguo, viti, magari na hata chakula. Mnanunua lakini hamuuzi vitu vyenu nje. Kwa hiyo mnauangusha uchumi wetu kila siku na kuwatajirisha wengine. Napata wakati mgumu kununua dola kila siku ili kuimarisha shilingi yetu”

Akiwa anashangiliwa kwa makofi na vifijo na wafuasi wake, Museveni ametangaza mipango ya kubadilisha mfumo wa elimu wa sasa nchini Uganda.

Imeandaliwa na mwandishi wa VOA Kennes Bwire, Uganda

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG