Raia kumi na watatu wa Tanzania, pamoja na raia mmoja wa China, walifukiwa na udongo katisiku ya Alhamisi baada ya mgodi mmoja kuporomoka katika mkoa wa Geita nchini Tanzania, walipokuwa wakiendelea na uchimbaji wa madini. Kufuatia hayo, BMJ Muriithi alizungumza na mwandishi wa habari wa kituo cha Channel 10, Valence Robert, na kwanza akamuuliza, mkasa huo ulitokea saa ngapi...