Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:00

Merkel: Hatma ya Nchi za Ulaya ‘iko mikononi mwetu’


Chansela wa Ujerumani Angela Merkel
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel

Merkel hata hivyo amesisitiza kuwa Ulaya itatengeneza njia yake ya mustakbali wa ushirikiano huo bila ya kujali tofauti zilizoko kati yao na kiongozi huyo mpya.

Maoni ya Merkel yamekuja kujibu habari zilizochapishwa kuhusu mahojiano ya Trump na vyombo vya habari yaliyowashtua baadhi ya viongozi wa Ulaya kwa vile alivyorudia tena kuushambulia umoja wa kujihami wa NATO na kusema kuwa namna Ujerumani ilivyokabiliana na tatizo la uhamiaji ulaya lilikuwa ni kosa la kihistoria.

“Nafikiri sisi watu wa Ulaya tunahatma yetu wenyewe katika mikono yetu na nitaendelea kuhimiza kuwa ni lazima sote tusimame pamoja. “Merkel amesema hilo akikusudia ushirikiano wa wanachama 27 wa Jumuiya ya Ulaya.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Berlin, amesema wanachama wa EU wataungana “katika kutokomeza ugaidi, kulinda mipaka yao na kuhakikisha usalama wa ndani ya nchi na pia kufikia soko la pamoja la biashara la digitali, kwa ajili ya kutengeneza ajira.

Ameongeza kusema kuwa maoni ya Trump kuhusu Ulaya yanajulikana.

“Rais mteule amesha ainisha maoni yake, hivyo basi atapoanza kazi—kitu ambacho sasa bado hajaanza, sisi tutashirikiana bila wasiwasi na uongozi mpya wa Marekani na wakati huo tutajua ni aina gani ya makubaliano tutayafikia," alisema.

Akizungumza na Jarida la The Times la Uiingereza na gazeti la Ujerumani Bild, Trump alisema Jumapili kwamba NATO imepitwa na wakati “kwa sababu ilikuwa imeundwa miaka mingi nyuma.” Pia alirejea malalamiko yake yaliyokuwa akiyatoa mara kwa mara wakati wa kampeni ya uchaguzi, kwamba NATO hawachangii kile wanachotakiwa kuchangia.”

Trump amesema, “Nafikiri (Merkel) amefanya kosa lililoleta msiba mkubwa kwa kuwaruhusu hawa wavunja sheria, unajua, kuwachukua watu wote hawa popote walipotokea.”

Wengi wa wahamiaji walioingia Ujerumani ni waislamu ambao walimiminika Ulaya wakikimbia vita, ugaidi na umaskini katika maeneo ya Syria, Iraq na Afghanistan.

Trump aliharakisha kusema kuwa siku zote alikuwa anampa heshima kubwa Merkel na alikuwa anamchukulia ni kiongozi mzuri. Lakini amesema Ujerumani “ilipata sura kamili” ya matokeo ya sera yake ya uhamiaji – akijaribu kurejea tukio la shambulizi la lori la Disemba kwenye soko la Krismasi lililouwa watu 12.

XS
SM
MD
LG